|
|
JE, UMEJUA JINSI |
[Read "The Wonderful Discovery" in Your Language ]
|
KILA SIKU UNAWEZA... KUWA MSHINDI KWA UWEZO WA ROHO MTAKATIFU 1. Kabla hujampokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wako, uliongoza maisha yako
mwenyewe. (Isaya 53:6) Sasa tuone jinsi... BIBLIA INAVYOTUAMBIA HABARI ZA ROHO MTAKATIFU Biblia inaserna: 1: Rohe Mtakatifu ni Mungu (Matendo
5:3-5) Biblia inatuonyesha sina tatu za watu, kwanza... 1 MTU ASIYE MKRISTO
|
|||||||||||||||||||||||||
![]() |
MTU ASIYE MKRISTO | |
|
|
Kiti cha enzi, yaani
cha utawala katika maisha |
|
|
|
Mimi mwenyewe binafsi | |
|
|
Yesu | |
1. Yesu yuko nje ya maisha yake.
2. Mtu asiye Mkristo hukaa kwenye kiti cha enzi, akitawala maisha yake
mwenyewe.
3. Huyu anahitaji kumpokea Yesu kuwa Mwokozi wake.
Mtu wa namna ya pili ni ...
Tunapompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wetu, Roho Mtakatifu huingia kukaa ndani yetu. (Warumi 8:9). Kujazwa Roho Mtakatifu, maana yake ni kumkubali Yesu kututawala na kutuongoza.
Biblia inseleza maisha yaliyolaa Roho Mtakatifu kama hivi:
"Tunda la Roho ni upendo, furaha,
amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi..." Wagalatia
5:22-23
"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi
mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na
Samaria, nata mwisho wa nchi."
Matendo Ya Mitume 1:8
Tunapokubali Yesu atawale maisha yetu, tutapenda. kumpendeza Mungu.
Picha hii inaonyesha
jinsi alivyo Mkristo aliyejazwa Roho Mtakatifu:
MKRISTO ALIYEJAA ROHO MTAKATIFU
| Huyu
Mkristo . . . * anaye Kristo moyoni. * anao uwezo wa Roho Mtakatifu * huleta wengine kwa Kristo * huomba hata kupata majibu. * hufahamu Neno la Mungu. * humtegemea Mungu. * humtii Mungu |
|
![]() |
Malshani
mwake yatonekana haya: * upendo * furaha * amani * uvumilivu * utu wema * uaminifu * upole |
1. Yesu yumo maishani mwake kama Mwokozi
wake.
2. Yesu Kristo yupo katika kiti cha enzi akiongoza.
3. Sasa yeye ni mtumishi anayemtii Yesu Kristo.
4. Kadiri Mkristo anavyojifunza kukubali Roho Mtakatifu amwongoze, matunda
ya Roho yatazidi kuonekana maishani mwake.
Lakini Mkristo asipojaa (tawaliwa) Roho Mtakatifu yeye
ni...
Mkristo mwenye tabia ya mwilini hufikiri zaldi juu ya kujipendeza kuliko kumpendeza Mungu. Hufanana na mtoto mchanga anayetaka mambo yake tu - kama watu wa dunia.
Biblia inasema haya juu ya Mkristo anayejipendeza,
"Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama
na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama
na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa, sikuwalisha chakula:
kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa
ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina,
je! si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenda kwa jinsi ya
kibinadamu?'
1 Wakorintho 3:1-3
Sasa tazama ...
Picha hii ni ya Mkristo
mwenye tabia ya mwilini
MKRISTO MWENYE TABIA YA MWILINI
| Mkristo
huyu: * hamtegemei Mungu kwa ukamilifu * mara nyingi hatii * havuti wengine kuja kwa Kristo * maombi si ya maana kwake * hapendelei sana kusoma Biblia * mawazo yake ni maovu mara nyingi |
|
|
|
Aweza
. . . * kuwa na wivu * kuwa na hatia moyoni * kuhangaika * kukata tamaa * kuhukumu wengine * kukasirika |
Ujue kwamba:
1. Yesu angali yumo maishani mwake kama Mwokozi
2. Mwenyewe huketi kitini na kutawala maisha yake.
3 Yesu hana utawala kamili.
Mkrlsto mwenyo table ya mwilini wakati mwlngine hutaka
kumpencleza
Mungu lakini ...
mare nyingi anataka kufanya mema asiweze ...
"Maana sijui nifanyalo; kwa sababu lile nilipendalo,
silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. Najua ya kuwa ndani
yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka
nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Ole wangu, maskini mimi! ni nani
atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?"
Warumi 7:15, 18, 24
Kutokana na hayo ...
Mkristo mwenye tabia ya mwilini hana maisha
ya furaha.
Huishi maisha ya kushindwa mara nyingi. Wakati mwingine hatendi
karna Mkristo hata kidogo.
Tukumbuke tuliyoyasoma kwa kutazama tena...
| ZILE AINA TATU ZA WATU | ||
| 1. Mtu asiye Mkristo | 2. Mkristo aliyejazwa Roho Mtakatifu | 3. Mkristo mwenye tabia ya mwilini |
![]() |
![]() |
![]() |
Wewe ni mtu wa namna ipi?
Ungependa kuwa Mkristo wa namna ipi?
JE, MKRISTO WA TABIA YA MWILINI AWEZAJE KUJAZWA (KUTAWALIWA) ROHO MTAKATIFU?
TWAJAZWA
(KUTAWALIWA) NA ROHO MTAKATIFU KWA IMANI
Twapata kuwa Wakristo kwa imani katika Yesu Kristo
Mwokozi wetu. Twajazwa Roho Mtakatifu kwa imani tukimtegemea Mungu na kutii
neno lake.
Unaweza kutueta hatua tatu ili kuonyesha imani yako sasa hivi.
1. WULISHE MUNGU KWAMBA
UNATAKA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU.
"Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa." Mathayo
5:6
2. UNGAMA DHAMBI ZAKO KWA MUNGU "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni
mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zertu, na kutusafisha na
udhalimu wote." I Yohana 1:9
Maana yake kuungama ni:
a. Unakubaliana na Mungu kwamba umefanya dhambi.
b. Unamshukuru Mungu kwa kukusamehe na kukusatisha kwa damu ya Yesu
Kristo.
c. Unaipa dhambi kisogo na kumtii Mungu, yaani kutubu.
3. JITOE KWA MUNGU
"Wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hal baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki." Wanimi 6:13
Kuishi maisha yaliyojaa (kutawaliwa na) Rho Mtakatifu, hatuna budi kukbali Yesu atawale kila tutendalo.
Lazima atawale matumizi ya pesa zetu, wakati wetu wa mapumziko, kazi yetu, uhusiano wetu na jamaa na marafiki na wengine.
Je, umefahamu hatua hizi tatu?
Je, tuzirudie tena?
UMTEGEMEE MUNGU AKUJAZE ROHO WAKE MTAKATIFU
Mungu atakujaza (kukutawala na
kukuwezesha) na Roho wake
Mtakatifu kama ukimtegemea akufanyie hivyo.
Kuna maneno mawili muhimu kukumbuka
1. UTII AGIZO LAKE
KUJAZWA
"Msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho."
Waefeso 5:18
2. TEGEMEA AHADI YAKE
KUKUJAZA
"Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake,ya kuwa,tukiomba kitu,sawasawa na
mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote,
twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba." I Yohana 5:14-15
Hata sasa...
UNAWEZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU KWA IMANI Njia moja kuonyesha imani yako ni kwa maombi. UNAWEZA KUOMBA HIVI:
Je, utapencla kumwomba Mungu akujaze na kukutawala na kuwezesha maisha yako? Je, ungependa kuomba sala hii sasa? KWA IMANI UNAWEZA KUJUA KWAMBA UMEJAA (KUTAWALIWA NA) ROHO MTAKATIFU Je, ulijitayarisha kama tulivyoeleza katika kurasa 12 hadi
14?
1. Mungu anakuagiza kwmba ujazwe Roho Mtakatifu. Ni ahadi yake
kukujibu unapoomba kulingana na mapenzi yake. UNAWEZA KUENDELEA KUJAZWA (KUTAWALIWA) NA ROHO MTAKATIFU Kama ukifanya dhambi tena kwa kuongoza maisha yako mwenyewe,
inakupasa kufanya mambo mawili. 1 . Ungama dhambi yako kwa Mungu. Yeye atakusamehe na
kukusafisha tena, (I Yohana 1:9).
Uipe dhambi hii kisogo na kumtii Mungu. 2. Unahitaji kujazwa (kutawaliwa na kupata nguvu) kwa Roho Mtakatifu tena. Mwombe Yesu Kristo kutawala maisha yako. Utii AGIZO la Mungu kujazwa Roho Mtakatifu. Tegemea AHADI ya Mungu kukujaza. Waefeso 5:18, 1 Yohana 5:14-15. Fuata njia hizi mbili kila mara Roho Mtakatlfu anapokuonyesha dhambi maishani mwako. Nawe utakuwa na maisha ya furaha na kuzaa matunda ya kiroho. UMTEGEMEE ROHO MTAKATIFU AENDELEE KUKUJAZA (KUKUTAWALA) HIVYO. NDIPO YESU KRISTO ATAKUWA KATIKA KITI CHA ENZI CHA MAISHA YAKO KILA SIKU. Unaweza kujua kwamba ... WAKATI ROHO MTAKATIFU ANAPOKUONGOZA NA KUKUTAWALA MAISHA YAKO: 1. Matunda ya Roho Mtakatifu yatazidi kuonekana katika maisha yako (Wagalatia 5:22-23). 2. Maombi yako yatazidi kusikika (Yakobo 5:6). 3. Utazidi kufahamu Biblia (2 Timotheo 3:16). 4. Utakuwa na uwezo wa Mungu kumshuhudia. (Matendo 1:8). 5. Utakuwa na uwezo wa Mungu kushinda majaribu na dhambi. (I Kor. 10: 13). 6. Utamwamini Mungu na ahadi zake (2 Petro 1:3-11). 7. Utaendelea kuishi maisha ya Mkristo aliyeujazwa Roho
Mtakatifu kwa imani 8. Utakuwa na ushind juu ya pepo wabaya (mashetani). (1 Yohana 4:1-4). Ni jambo muhimu... KWENDA KANISANI Biblia inatuambia kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25) Ebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikilundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kaishi maisha ya kikristo peke yako. Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani. Uhudhurie kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa. Kama kweli hii imekusaidia ... UKISOME KIJITABU HIKI NA KUMPA MWINGINE The Life Ministry P.O. Box 21417 Nairobi, Kenya |
|
|
| © 1995-2001 Campus Crusade for Christ International Questions and Comments are always welcome! http://www.jesuswho.org/spirit/swahili-kenya/default.htm webmaster@jesuswho.org last updated: 18-08-2006 |
|